TotalEnergies yasaidia kuimarisha elimu ya mtoto wa kike

DODOMA-Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd kwa kushirikiana na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo Novemba 22,2024 imekabidhi katoni 360 za taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni 25.5 kwa shule nne za sekondari.
Shule za sekondari zilizonufaika na msaada huo wa taulo za kike ni Lemura ya Hai, Kilimanjaro, Sitalike ya mkoani Katavi, Manunus Mkombozi ya Same, Kilimanjaro na Isack Kamwelwe ya mkoani Katavi. Zaidi ya wanafunzi 1,200 watanufaika kwa mwaka mzima.
Mwaka huu kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa imetoa jumla ya Katoni 500 za taulo za kike zenye thamani ya Sh. Milioni 35.4. Pia imetoa Madawati 200 yenye thamani ya Sh. Milioni 25.9 kwa shule za tatu za mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi ya Elimu -TEA Bw. Masozi Nyirenda, ameishukuru kampuni hiyo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano ya Kampuni - TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd, Bi. Getrude Mpangile ameahidi kuwa kampuni yake itaendelea kuwekeza katika sekta ya elimu.
Bw. Philipo Silvester Mwalimu Mkuu kutoka Shule ya Sekondari Lemura na Glory Micheal mwalimu wa Shule ya Sekondari Manunus -Mkombozi wamesema msaada huo utasaidia kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi wa kike. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news