DAR-Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza rasmi kwamba Young Africans Sports Club (Yanga SC) itatumia Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa mechi zake zilizosalia za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu huu wa 2024/25.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya TPLB ambayo imetolewa leo ikifafanua kuwa, Klabu ya Yanga imetekeleza taratibu zote za kuutumia uwanja huo ikiwemo kupata ridhaa na kuingia makubaliano na wamiliki wa dimba hilo.
Bodi ya Ligi pia imefanya mabadiliko ya ratiba kwa mechi tatu za NBC Premier League. Mchezo wa Azam FC dhidi ya Singida BS, sasa utachezwa Novemba 28, badala ya Novemba 27, 2024.
Mchezo kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Azam FC, sasa utapigwa Desemba 1, badala ya Novemba 30, 2024.
TPLB pia imetangaza kuondoa mchezo kati ya Singida Black Stars dhidi ya Simba ambao ulipangwa kuchezwa Desemba 1, 2024, sasa utapangiwa tarehe nyingine.
Tags
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania
Habari
KMC Complex
Ligi Kuu ya NBC
Michezo
Yanga SC
Young Africans Sports Club