ZANZIBAR-Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema,kufanyika kwa tunzo za Trace nchini itachangia kuongeza idadi ya watalii na jukuza uwekezaji.
Amesema hayo katika Hoteli ya The Mora, Matemwe wakati wa utambulisho wa tunzo za Trace Awards zinazotarajiwa kufanyika Zanzibar kwa mwaka 2025.
Amesema,ujio wa tunzo hizo za Kimataifa utachangia jukuza vipaji na kuhamasisha mashirikiano ya wadau wa Tasnia ya Muziki nchini.
Ameongeza kuwa, tunzo hiyo ni zaidi ya burudani, kwani inaweza kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi hivyo amewataka kijana kujiandaa kuchangamkia fursa hiyo.
"Hili ni jambo kubwa, ni jambo la kihistoria. Ni heshima kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, baada ya tukio hili tunaongeza kiwango cha watalii wanaokuja Zanzibar."
Kwa upande wake Mtayarishaji kutoka Trace Music Awards, Serveb Mosha amesema,tuzo hizo ni muhimu katika kuikuza tasnia ya nuziki na kuendeleza vipaji kutoka Afrika ambapo kwa mwaka 2025 wamedhamiria kuutangaza Muziki wa Bongo Fleva Duniani.
Zaidi ya watu 3,000 kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki kwenye tuzo hizo ambazo ni mara ya kwanza zitafanyika Zanzibar kuanzia Febuari 24 hadi 26,2025.
Tuzo za Trace Awards zilianzishwa kwa mara ya kwanza Oktoba 21, 2023 kwa ajili ya kuutangaza Muziki wa Afrika na Wasanii wa Afrika waliopo ndani na nje ya Afrika.