Tutaendelea kuifanya Sekta ya Fedha kuwa imara,thabiti na stahimilivu-BoT

NA GODFREY NNKO

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema, ikiwa msimamizi wa taasisi za fedha nchini itaendelea na jukumu la kuhakikisha Sekta ya Fedha inakuwa imara,thabiti na stahimilivu ili kuwezesha shughuli za uchumi kupatikana kwa wakati na kwa usahihi.
Hayo yamesemwa leo Novemba 14,2024 jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja wa Huduma Ndogo za Fedha,Dickson Gama wakati akifungua mafunzo kwa wahariri na waandishi wa habari kuhusu usimamizi wa mikopo ya mitandaoni.

Amesema, semina hii ina umuhimu mkubwa kutokana na ongezeko la huduma za utoaji mikopo mitandaoni pamoja na changamoto zake.

"Na ni jukumu la Benki Kuu katika kusimamia Huduma Ndogo za Fedha nchini.

"Hivyo, kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari kama kiunganishi kati ya Benki Kuu na jamii ya Watanzania na Dunia kwa ujumla. Benki Kuu imeandaa semina hii kwa wahariri na waandishi wa habari kwa lengo la kujenga uelewa mzuri zaidi.

"Ni katika utekelezaji wa sheria na kanuni za Huduma Ndogo za Fedha na jukumu letu sisi kama msimamizi wa sekta hii pamoja na huduma ndogo ya huduma za fedha."

Amesema, mikopo ya mitandaoni imekuwa ni sehemu ya mfumo wa fedha, kwani imerahisisha utoaji wa huduma za mikopo kwa urahisi na kasi zaidi.

"Hata hivyo, ukuaji huu wa haraka umesababisha changamoto kadhaa ikiwemo masuala ya kimaadili, riba na gharama kubwa za mikopo na kukosekana kwa taarifa."

Amesema, kutokana na changamoto hizo ndiyo maana wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ili kuifanya huduma hiyo kuwa na manufaa kwa wananchi hasa baada ya mtoa mikopo kuidhinishwa na BoT.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news