DAR-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema, Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2023/24 inalenga kukuza lugha ya Kiswahili, kutangaza na kuhifadhi utamaduni wa Kitanzania.

Ameongeza kuwa, pamoja na azma hiyo Serikali imedhamiria kuhamasisha ushiriki wa Waandishi bunifu kuwania Tuzo hizo ili kukuza uandishi na kuchangamsha Soko la vitabu nchini.
"Tunapokuwa na vitabu vizuri, vilivyoandikwa kwa Kiswahili, tunaamini watu watavipenda, hivyo tungepenga tuwe na Waandishi wengi ambao baadae vitabu vyao vitatafsiriwa kwa lugha mbalimbali na kutangaza utamaduni wetu,"amesema Prof.Mkenda.
Amewahimiza Waandishi bunifu kuwasilisha miswaada kuwania Tuzo hizo zinazoshindaniwa katika tanzu za Riwaya, Ushairi, Hadithi za Watoto na Tamthilia.

Ameeleza kuwa Kamati imeongeza muda wa kupokea Miswada hivyo Dirisha la kuwasilisha litakuwa wazi hadi Disemba 31, 2024,
Waandishi Bunifu mnakaribishwa kushiriki katika Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2024/25.