Ujuzi ni nyenzo muhimu katika Sekta ya Utalii-Profesa Mkenda

ARUSHA-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema ni muhimu kuunganisha taaluma na viwanda katika sekta ya utalii na ukarimu ili kufungamanisha maarifa ya kitaaluma na ujuzi ili kuziba pengo la wahitimu wasio na ujuzi stahiki.
Mkenda ametoa kauli hiyo Novemba 22, 2024 jijini Arusha katika kilele cha Kongamano la Kimataifa la Kuunganisha Taaluma na Viwanda katika Sekta ya Utalii na Ukarimu, ambapo amesema kuwa ili kufikia azma hiyo Serikali imeanzisha mfumo mpya wa elimu ya sekondari wenye mkondo wa elimu ya jumla na mkondo wa Amali ikijumuisha mafunzo ya ufundi na ufundi stadi.
Aidha, Prof. Mkenda amesisitiza kuimarisha ushirikiano wa karibu kati ya vyuo na sekta ya viwanda pamoja na kudumisha ushirikiano wa kimataifa ili kuboresha sekta ya utalii na ukarimu ikiwa ni pamoja na kuzalisha wataalam mahiri kwa maendeleo ya taifa na kikanda.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania, Bi. Jesca William amesema kongamano hilo lililoongozwa na kaulimbiu: "𝗞𝘂𝘂𝗻𝗴𝗮𝗻𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗧𝗮𝗮𝗹𝘂𝗺𝗮 𝗻𝗮 𝗩𝗶𝘄𝗮𝗻𝗱𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗦𝗲𝗸𝘁𝗮 𝘆𝗮 𝗨𝘁𝗮𝗹𝗶𝗶 𝗻𝗮 𝗨𝗸𝗮𝗿𝗶𝗺𝘂." Litasaidia kuimarisha mafunzo katika sekta ya utalii na ukarimu pamoja na kukuza sekta hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news