Utoaji wa huduma za jamii unaboreshwa ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo-Mtwale

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale amesema, Ofisi ya Rais-TAMISEMI inaendelea kuboresha utoaji wa huduma za jamii kwa kushirikiana na wizara za kisekta ili kukuza uchumi, kuleta maendeleo na kuimarisha ustawi wa mwananchi mmoja mmoja na wa taifa kwa ujumla.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale akizungumza na washiriki wa kikao kazi cha Wizara za Kisekta (hawapo pichani) kilichofanyika katika Ukumbi Mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, kilicholenga kujadili uratibu wa mipango na bajeti kwa shughuli zinazotekelezwa na Wizara za Kisekta katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Bw. Mtwale amesema hayo leo katika Ukumbi Mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara za Kisekta kilicholenga kujadili uratibu wa mipango na bajeti kwa shughuli zinazotekelezwa na kusimamiwa katika ngazi za Halmashauri, Mikoa na Wizara za Kisekta.

“Kikao hiki ni fursa ya kujadili mipango na bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26, hivyo niwaombe mshiriki kikamilifu kwa kutoa maoni na ushauri utakaowezesha uandaaji mzuri wa mipango na bajeji kwa mwaka wa fedha ujao,” Bw. Mtwale amesisitiza.
Washiriki wa kikao kazi cha Wizara za Kisekta (hawapo pichani) wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi hicho, kilichofanyika katika Ukumbi Mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma ili kujadili uratibu wa mipango na bajeti kwa shughuli zinazotekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Sanjari na hilo, Bw. Mtwale amesema kikao hicho kitasaidia kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Serikali katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika ngazi za Mikoa na mamlaka za Serikali za Mitaa.

Aidha, Bw. Mtwale amewataka washiriki kuongeza ubunifu wakati wa uandaaji wa mipango na bajeti ili kutengeneza mazingira wezeshi kwa wananchi na sekta binafsi, na hatimaye kuongeza thamani ya mazao na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ambazo zitakuwa na bei nzuri katika masoko ya nje.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. John Cheyo akieleza lengo la kuandaa kikao kazi cha Wizara za Kisekta kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale kufungua kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi Mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma.

“Nitumie fursa hii kuendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza mhakikishe kuwa, mnaandaa mipango na kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa afua na shughuli mbalimbali katika ngazi za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa,” Bw. Mtwale amehimiza.

Naye, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. John Cheyo amesema lengo la kuandaa kikao cha wizara za kisekta ni kujenga mahusiano mazuri kiutendaji pamoja na kuangalia namna bora ya kusaidiana katika kutekeleza shughuli za kisekta kwa wananchi katika ngazi ya chini ambayo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale akiwa katika kikao kazi cha Wizara za Kisekta kilichofanyika katika Ukumbi Mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, ili kujadili uratibu wa mipango na bajeti kwa shughuli zinazotekelezwa na Wizara za Kisekta katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Wizara za Nishati, Kilimo, Maji na Mifugo na Uvuvi ambazo zimewakilishwa hapa zina shughuli za kisekta zinazotekelezwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zipo chini ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, hivyo tumeona ni muhimu tukakutana ili kupata namna bora ya kuratibu utekelezaji wa shughuli hizo,” Bw. Cheyo amefafanua.

Kikao kazi hicho cha siku moja ambacho ni muendelezo wa kikao kilichofanyika mwaka wa fedha 2023/24, kimeudhuriwa na Wakurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara za Kisekta na taasisi zake pamoja na Wataalam kutoka ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news