BRUSSELS-Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amekiri waziwazi kuhusu matatizo makubwa yanayokikabili Chadema katika maandalizi ya kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa.
Katika mahojiano na mwanahabari Chief Odemba, Lissu ameonyesha jinsi chama hicho kinavyokumbana na changamoto kubwa katika kukusanya rasilimali fedha, watu na vifaa.
Hali hii inadhihirisha wazi kwamba Chadema hawana uwezo wa kujiandaa ipasavyo kwa ajili ya uchaguzi.
Ingawa Chadema wanakiri sasa kwamba hawawezi kukusanya fedha, rasilimali, au watu wa kutosha kuendesha kampeni yenye mafanikio, ni wazi kuwa watakapopata matokeo ya uchaguzi, wataendelea kudai kwamba uchaguzi huo umeporwa kwao.
Hii inadhihirisha jinsi Chadema wanavyoshindwa kukubali ukweli na badala yake wanageuza kila kipande cha kushindwa kuwa kisingizio cha kudai udanganyifu.
Wananchi wanapaswa kuangalia kwa makini na kuelewa kwamba Chadema wanajenga mazingira ya kutafuta huruma badala ya kujiandaa kwa ushindani wa haki.
Haya yanajiri ikiwa, Lissu pia anatajwa kuwa miongoni mwa viongozi wa chama ambao hawakujiandikisha katika daftari la mkazi kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa.
Zoezi ambalo lilifanyika mwezi uliopita kote nchini kwa ajili ya uchaguzi huo wa Novemba 27,2024.
Tags
Habari