KILIMANJARO-Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) mkoani Kilimanjaro imeendelea kukoleza kasi ya kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji safi na salama katika kila kona ya mji.
Kwa sasa,MUWSA wanaendelea na kazi ya uchimbaji wa visima 900 ambapo leo Jumapili ya Novemba, 2024 wamepata mtambo wa kuchimba kisima kirefu.
Ni katika Kitongoji cha Shabaha kilichopo Kata ya Mabogini ambapo wamepata maji ndani ya mita 95.
"Hakika tumedhamiria kutatua changamoto za wananchi tunaowahudumia."