SEOUL-Vijana mabaharia watano kutoka Tanzania wamemaliza mafunzo ya miezi miwili na nusu ya melini (on board training) nchini Korea Kusini katika chuo cha Korea Maritime and Fishing Technologies (KIMFT).
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Korea Kusini,Mheshimiwa Togolani Edriss Mavura ameeleza kuwa,mafunzo hayo yalishirikisha nchi 13.
"Mabaharia hawa wahitimu wa Chuo cha Mabaharia Tanzania (DMI) ni awamu ya pili ya washiriki.
"Awamu ya kwanza ya mabaharia wanne walishiriki mafunzo haya mwaka jana na wote wakapata kazi katika meli za kimataifa.
"Fursa hii ni matokeo ya juhudi za Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini kuunganisha KIMFT na Chuo cha Bahari Tanzania ambapo taasisi hizi mbili zilisaini MoU mapema mwaka jana."