ARUSHA-Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Ngazi ya Wataalam umeanza jijini Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano huo utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2024.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Haji Janabi akiongoza kikao kwa niaba ya Mwenyekiti, Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao. Kikao hicho cha ngazi ya wataalam kimefanyika jijini Arusha kuandaa Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2024. Kikao cha Wataalaam kitafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba 2024 na kufuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu mnamo tarehe 26 Novemba 2024.
Pamoja na mambo mengine, mkutano wa wataalam unajadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya mtangamano wa Jumuiya hiyo ambazo baadaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya Mawaziri.
Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Benjamin Mwesiga akichangia jambo wakati wa kikao cha Wataalam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Abdilah Mataka akifuatilia kikao.
Sehemu ya ujumbe wa Burundi wakishiriki Mkutano wa Wataalam.
Ujumbe wa Kenya.
Ujumbe wa Somalia.
Ujumbe wa Uganda.
Sehemu ya Wajumbe wakishiriki kikao cha wataalam.
Sehemu nyingine ya wajumbe wakati wa kikao.
Taarifa zilizopokelewa na kujadiliwa ni pamoja na Taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya awali ya Baraza la Mawaziri; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu masuala Forodha, Biashara na masuala ya kifedha; Taarifa kuhusu Miundombinu, Sekta za Uzalishaji, Sekta za Kijamii na masuala ya Kisiasa; Taarifa kuhusu masuala Fedha na Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya.
Mkutano wa Ngazi ya Wataalam umeongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Haji Janabi kwa niaba ya Mwenyekiti, Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao.
Mkutano huu wa ngazi ya wataalam unafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba 2024 ukifuatiwa na mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 26 Novemba 2024 na tarehe 27 na 28 Novemba 2024 utafanyika Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri ambao utapokea agenda mbalimbali kutoka kwa Makatibu Wakuu.
Wajumbe wakishiriki kikao.
Ujumbe wa Tanzania wakishiriki kikao.
Kikao kikiendelea.
Wajumbe wakati wa kikao.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Agenda zitakazojadiliwa katika Baraza la Mawaziri zitawasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Novemba 2024 kwa ajili ya kupitishwa na kuridhiwa kwa utekelezaji.
Nchi nane Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki za Burundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda zinashiriki mkutano huo.