DODOMA-Baada ya zoezi uchukuaji na urejeshaji wa fomu jumla ya wagombea walioteuliwa baada ya mchakato wa rufani kwa kila nafasi kwa vyama vyote 19 vyenye usajili kamili ni kama ifuatavyo;
Mwenyekiti wa Kijiji 18,340: Mwenyekiti wa Mtaa 7,545: Mwenyekiti wa Kitongoji 85,522: Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi Mchanganyiko) 160,371:
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa ameyasema hayo usiku wa Novemba 28,2024 wakati akitangaza matokeo ya jumla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi la Wanawake) 108,166: Wajumbe wa Kamati ya Mtaa (Kundi Mchanganyiko) 18,552 na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa (Kundi la Wanawake) 11,762.