Wakulima walipwe fedha zao kutokana na kilo walizopeleka ghalani-Mrajis

MTWARA-Vyama Vikuu vya Ushirika vinavyowasimamia wakulima wa zao la Korosho nchini, vimetakiwa kuacha kuwapunja malipo yao wakulima wa zao hilo, kwa kisingizio cha mazao kupungua ghalani baada ya kupimwa kutokana na sababu zisizoeleweka.
Agizo hilo limetolewa na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, leo Novemba 10, 2024 mkoani Mtwara, wakati akizungumza na viongozi wa vyama hivyo kutoka Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Pwani.

Amesema, Viongozi wa Vyama Vikuu wanatakiwa kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao kutokana na kilo walizopeleka ghalani na si vinginevyo, na si wajibu wao kukatwa gharama zozote zisizotambulika na ambazo hazijawekwa kwenye utaratibu unaotambulika na Serikali.

"Mkulima alipwe malipo yake kutokana na kile alichokileta ghalani na si vinginevyo, kama kuna changamoto yoyote aambiwe hapo hapo na si Mkulima ameshakabidhi Korosho zake na baadae anakatwa fedha kutokana na sababu zisizoeleweka," amesema.

Dkt. Ndiege amesema wapo wanaodai kuwa wakulima wanakatwa fedha hizo kwa kisingizio cha Korosho kupungua kutokana na unyaufu, jambo ambalo amesema haiwezekani na vyama vya msingi havitakiwi kupokea Korosho zenye changamoto hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news