WANANCHI 26,963,182 WAPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

DODOMA-Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura lilifanyika kuanzia tarehe 11 mpaka 20 Oktoba, 2024 ambapo jumla ya wapiga kura 31,282,331 walijiandikisha. Kati yao, wanawake walikuwa 16,045,559 na wanaume walikuwa 15,236,772.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa ameyasema hayo usiku wa Novemba 28,2024 wakati akitangaza matokeo ya jumla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mohammed Mchengerwa.

Aidha, kwa mujibu wa kanuni ya 12 ya Tangazo la Serikali Na. 571, 573 na 574 na Kanuni ya 11 ya Tangazo la Serikali Na. 572 kulikuwa na muda wa wananchi kuweka pingamizi kwa wananchi waliojiandikisha. Baada ya kushughulikia pingamizi wapiga kura waliohakikiwa kwa ajili ya kupiga kura walikuwa 31,255,303.

Pingamizi za uandikishaji zilitokana na sababu mbalimbali ikiwemo wananchi kutokuwa wakazi wa maeneo husika na wengine kujiandikisha kwenye maeneo wanayofanya shughuli zao za kiuchumi badala ya maeneo yao ya makazi.

Aidha, wananchi waliopiga kura siku ya tarehe 27 Novemba, 2024 ni 26,963,182 sawa na asilimia 86.36 ya wananchi waliokuwa na sifa ya kupiga kura.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news