Wanawake wajasiriamali Dodoma wamshukuru Rais Dkt.Samia kwa fursa za kiuchumi

𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀-Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoani Dodoma kwa kauli moja limempongeza,Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza mazingira mazuri ya ukuaji wa kiuchumi wa wanawake pamoja na kuongeza fursa za kiuchumi mkoani Dodoma ambapo wananwake ni kundi kubwa wanufaika.Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa,Bi. Maryrhobi Mabhaya wakati wa Kongamano la wakina Mama wa Dodoma kumpongeza Mh. Rais Samia kwa namna ambavyo serikali ya awamu ya sita ilivyochochea maendeleo katika Mkoa wa Dodoma na hivyo kutengeneza fursa kubwa ya kiuchumi.
“Dodoma ya leo sio kama ya zamani,maendeleo ya Dodoma ya sasa huwezi kuyasema bila kumtaja Rais Samia.

"Hivi sasa kuna fursa lukuki za kiuchumi ambazo wakinamama tukizitumia vizuri zitasaidia kubadilisha uchumi wa wakina mama wa Dodoma.Sisi kama Jukwaa malengo yetu ni kujenga eneo la maduka makubwa“Shopping Mall“ pamoja na kuwa na eneo maalum la biashara ta wakina mama,“amesema Maryrhobi.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mlezi wa Jukwaa Mama Tunu Pinda amesema ni wakati sasa wanawake wa Dodoma kutumia fursa hizi kubwa kiuchumi ambazo Mh. Rais Samia amekuwa kinara wake kuzitengeneza hapa Dodoma ili kujiimarisha na kukua zaidi kiuchumi.
Akiwasilisha hotuba yake,Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amesema tangu maamuzi ya kuhamishia shughuli za serikali Dodoma,fursa nyingi za kiuchumi zimeongezeka na hivyo serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuliona kundi kubwa la wanawake likinufaika kupitia sheria na sera wezeshi.

Mavunde alieleza kwamba,Mheshimiwa Rais Samia amerudisha mikopo ya wakina mama ya 10% na pia Sheria ya Manunuzi ya Umma imefanyiwa marekebisho ili Taasisi nunuzi zitenge 30% ya manunuzi yake kwa ajili ya makundi maalum likiwemo kundi la wakina mama.

“Nitaendelea kuunga mkono jitihada za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa vitendo,na mwaka huu nitakabidhi kwa kikundi cha wakina Mama Ipagala mitambo ya kusafisha mafuta ya Alizeti ambapo ni sehemu ya ahadi yangu ya uanzishwaji wa kiwanda cha kuongeza thamani mazao kila mwaka,“amesema Mavunde.
Wanawake wa Dodoma walitumia jukwaa hilo pia kumpa tuzo ya Mh. Anthony Mavunde kwa kutambua mchango wake mkubwa kuwaendeleza wakina mama mkoani Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news