Watu 29 wafariki ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo

DAR-Serikali imesema idadi ya vifo vilivyotokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Mtaa wa Manyema na Mchikichini Kata ya Kariakoo jijini Dar es Salaam vimefikia 29.
Ajali hiyo ilitokea Novemba 16,2024 ambapo Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliendesha zoezi la uokoaji wa watu waliokwama kwenye jengo hilo.

Akizungumza leo Novemba 26,2024 Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba amesema idadi ya vifo vilivyotokana na kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo imefikia 29 hadi kufikia leo.

Makoba amesema,lipo pia zoezi linaloendelea la kutambua miili mingine kwa kutumia teknolojia ya vinasaba kwa maana ya DNA na wakishathibitisha watatoa taarifa.

"Mpaka kufikia muda huu ambao tunazungumza kwa bahati mbaya namba ya marehemu ambao tumethibitisha ni 29, kwa hiyo namba imeongezeka kidogo tunaendelea kuwaombea wenzetu wapumzike kwa amani.

“Lipo zoezi linaloendelea la kutambua miili mingine kutumia teknolojia ya vinasaba (DNA) na wenyewe tutatoa taarifa tukishathibitisha ndugu pamoja na miili ya wenzetu, kwa upande wa majeruhi idadi ipo palepale.”

Awali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan alisema Serikali itabeba gharama za matibabu kwa waliojeruhiwa pamoja na mazishi ya waliofariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news