Watu 84 waokolewa,13 wafariki dunia ajali ya kuporomoka ghorofa Kariakoo

BRAZIL-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema kuwa,hadi kufikia Novemba 17,2024 majira ya saa 4 asubuhi watu 84 wameokolewa na kufikishwa katika hospitali kwa ajili ya matibabu, huku majeruhi 26 wanaendelea na matibabu.
Ni kutokana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa nne katika Kata ya Kariakoo jijini Dar es Salaam tarehe 16 Novemba,2024.

Pia,Rais Dkt.Samia amebainisha kuwa, mpaka sasa watu 13 wamepoteza maisha katika tukio hilo, huku akieleza kuwa Serikali itabeba gharama za matibabu kwa wote waliojeruliwa pamoja na kuhakikisha waliofariki wanastiriwa vizuri.

“Nitoe pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na tukio hili, niwaombe watanzania wote tuwaweke wote katika maombi walioathirika na tukio hili, tuwaombee pumziko la amani wote waliopumzika mbele ya haki.”

Amesema kuwa, mpaka sasa hakuna sababu za kitaalamu za jengo hilo kuporomoka kwani kwa sasa kipaumbele ni kuwaokoa watu waliokuwa ndani ya jengo.

“Serikali itaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu zoezi la uokozi hadi litakapokamilika, tunavipongeza na kuvishukuru vyombo vyote vya usalama vinavyoendelea na zoezi la ukoaji wa ndugu zetu pamoja na mashirika binafsi waliojitolea na kutoa ushirikiano.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news