Watu tisa wa familia moja wafariki dunia kwa kusombwa na maji Tarime

MARA-Watu tisa wa familia moja wamefariki dunia mkoani Mara baada ya nyumba zao kusombwa na maji.
Ni kufuatia mvua kubwa kunyesha na kusababisha Mto Mori kujaa maji na kisha maji hayo kuelekea kwenye makazi ya watu.

Mto Mori upo mkoani Mara ambapo maji yake huwa yanaingia katika Ziwa Viktoria na hatimaye yanaelekea Bahari ya Kati kupitia Mto Naili.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 25, 2025 katika Mtaa wa Bugosi Halmashauri ya Mji wa Tarime ambapo makazi ya familia hiyo yalisombwa na maji huku mashamba na mali zingine zikiharibika.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele amesema familia hiyo ilikuwa na watu 11, ambapo wawili waliokolewa na tisa ndio waliosombwa na maji na kufariki dunia.

Meja Gowele amesema, miili nane kati ya tisa imepatikana, huku jitihada za kutafuta mwili mwingine zikiendelea.

Amefafanua kuwa, waliokumbwa na kadhia hiyo ni kaya mbili tofauti ambapo kaya moja yenye watu tisa imenusurika na moja yenye watu 11 imepoteza watu tisa.

Diwani wa Kata ya Nyamisangura, Thobias Elias Ghati amesema miili yote tisa imepatika na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Tarime, kilomita chache kutoka eneo la tukio.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news