Waziri Mkuu afanya mazungumzo na Dkt.Mehmet

DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 13, 2024 amefanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki ambaye anamaliza muda wake nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu, Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao Mheshimiwa Majaliwa amemsihi Balozi Mehmet kuendelea kuwa balozi mzuri wa Tanzania popote atakapokuwa sababu tayari anajua fursa za uwekezaji na utalii zilizoko nchini.
Kwa upande wake Balozi huyo ameshukuru Ushirikiano ambao ameupata kutoka Serikalini katika kipindi chake jambo ambalo limechangia kuimarisha Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news