Waziri Mkuu awasili Songea kushiriki Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya UKIMWI Duniani
RUVUMA-Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Novemba 30, 2024 amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea ambapo kesho Disemba 1, 2024 atashiriki katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya UKIMWI Duniani.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa ni Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango.