DODOMA-Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) amemuumbua Mbunge wa Kisesa, Luhaga Joelson Mpina kwa kulidanganya Bunge, jambo lililopelekea Mbunge huyo kuomba radhi na kufuta kauli zake zilizojaa upotoshaji na ubabaishaji.
Akitoa ufafanuzi juu ya jambo hilo Dkt.Nchemba amesema, hakuna taasisi au kampuni binafsi yoyote inaruhusiwa kukusanya kodi na mapato yote yanakusanywa na TRA na TPA, toka Kampuni ya DP World kuanza shughuli zake ufanisi umeongezeka sana, makusanyo ya bandarini nayo yamepaa hadi Trilioni 1.23 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa toka TRA ianzishwe.
Baada ya ufafanuzi huo, Dkt.Nchemba alimtaka Mbunge huyo kufuta kauli zake za uongo na kuomba radhi na Mpina alikiri na kufanya hivyo.
Awali Mbunge huyo aliliongopea Bunge kwa kusema Kampuni ya DP World inakusanya kodi bandarini.
Naibu Spika, Mhe. Zungu ametumia fursa hiyo kumpongeza Waziri wa Fedha kwa kutoa ufafanuzi mzuri unaoeleweka na kuwataka Mawaziri wengine kuiga mfano wake ili kudhibiti upotoshaji ndani ya Bunge.
Tags
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Habari
Mwigulu Lameck Nchemba Madelu
Wizara ya Fedha Tanzania