DAR-Wenyeviti 959 wa Serikali za Mitaa wamekula kiapo cha utii na uaminifu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Janeth Boaz Kinyage ili waweze kuwa na sifa ya kwenda kuwatumikia Watanzania.
Akizungumza katika zoezi hilo jijini humo, Hakimu Kinyage amewapongeza viongozi hao kwa kupewa dhamana na wananchi ili kwenda kuwatumikia katika mitaa yao.
Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi na Mkurugenzi wa hiji hilo, Elihuruma Mabelya amewasihi viongozi hao wakashirikiane na wananchi katika masuala mbalimbali ikiwemo utatuzi wa changamoto zao.
"Naipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya usimamizi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaelekeza wasimamizi wa uchaguzi wazingatie 4R hususani katika kulinda amani na utulivu uliopo hapa nchini,"amesema Mabelya.
Zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lilitekelezwa Novemba 27,2024 ambapo Watanzania walipata fursa na haki ya kikatiba ya kuwachagua viongozi hao.