DAR-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imetozwa faini ya shilingi milioni 10 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kosa la kupitia mlango usio rasmi.
Ni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo wa Derby ya Kariakoo, kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:21 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Aidha, Klabu ya Yanga imetozwa faini ya shilingi milioni moja kwa kosa la kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia nguo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo wa Yanga dhidi ya Simba, kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Vilevil, Klabu ya Yanga imetozwa faini ya shilingi milioni moja kwa kosa la kuwakilishwa na kocha mkuu pekee kwenye mkutano wa wanahabari kuelekea mchezo wa Derby ya Kariakoo, kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:58 ya Ligi Kuu.
Ni kuhusu Taratibu za Mchezo inayotaka aambatane na nahodha ama mchezaji mwenye ushawishi kikosini.