Zanzibar itajenga uwanja mpya wa mpira kwa AFCON2027-Rais Dkt.Mwinyi

SHANGHAI-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameendelea na ziara ya kikazi nchini China ambapo leo amekutana na kampuni mbalimbali zinazolenga kuwekeza Zanzibar.
Katika mwendelezo wa ziara hiyo Rais Dkt. Mwinyi pia, amekutana na uongozi wa kampuni maarufu na yenye uzoefu wa miaka mingi, China Railway Construction Engineering Group (CRJE), yenye makao makuu Beijing, China katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Westin mjini Shanghai, China.
Katika mkutano huo, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kujenga Mji wa Kiserikali ambapo Serikali na taasisi zake zitawekwa sehemu moja ili kuboresha ufanisi na utendaji serikalini pamoja na kurahisisha huduma kwa wananchi.

Rais Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali pia ina mpango wa kujenga kiwanja cha mpira wa miguu cha kimataifa kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.

Mkutano huo umekutanisha Benki na taasisi za fedha, wakiwemo wenyeji CRJE, China Dasheng Bank of Tanzania, Jiangsu Financial Leasing Co. Ltd, Huaxia Bank, Citic Bank, na Bank of Shanghai, ambao wamekuja kujadili fursa za uwekezaji na ushirikiano wa fedha katika miradi mbalimbali ya maendeleo Zanzibar.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kushirikiana na wadau wote wa fedha na wawekezaji ili kufanikisha miradi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news