Zoezi la kupiga kura kwa washiriki wa Samia Kalamu Awards, tazama orodha ya waandishi wateule na vyombo vya habari hapa

DAR (Novemba 11,2024)-Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), tunapenda kuwajulisha wananchi na wadau wa habari kwamba zoezi la upigaji kura kwa washiriki wa "Samia Kalamu Awards" linaanza rasmi leo Novemba 11 na kumalizika Novemba 20, 2024.
Zoezi la upigaji kura litawahusisha wananchi ambao ndio walaji wamaudhui watakao changia asilimia 60 ya matokeo wakati asilimia 40 ya alama ya vigezo vya kitaaluma zimetolewa na jopo la majaji, na sasa ni zamu ya wananchi kufanya maamuzi ya mwisho kwa kupiga kura.

Watakaopigiwa kura ni wanahabari na vyombo vya habari vilivyokidhi vigezo vya kitaaluma vya uandishi wa habari za maendeleo.

Tuzo hizo zenye kauli mbiu "Uzalendo Ndio Ujanja" zimegawanywa katika makundi makuu matatu ambayo ni Tuzo Maalumu za Kitaifa, Tuzo za Vyombo vya Habari na Tuzo za Kisekta.

Makala 1,131 ziliwasilishwa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kuwania Tuzo hizi na baada ya uchambuzi wa kitaaluma kazi 85 zilizokidhi vigezo zimewekwa kwenye tovuti ya www.samiaawards.tz, na katika mitandao ya kijamii ya Instagram (samiakalamuawards), YouTubena Facebook (Samia Kalamu Awards), ili kuruhusu wananchi kuziona na kuzipigia kura kwa kuzingatia ubora na mchango wa makala hizo katika maendeleo ya taifa.

Ili kupiga kura kupitia tovuti ya www.samiaawards.tz fungua tovuti hii,utaona orodha ya kazi zinazoshindanishwa kwenye;


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news