Aishi Manula akwama kwenda Algeria kwa sababu za kiafya

DAR-Mlinda mlango wa Simba Sports Club,Aishi Manula ameshindwa kusafiri na timu ya Simba baada ya kupata changamoto za afya akiwa na wachezaji wenzake Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tayari kwa safari ya Algeria.
“Mlinda mlango Aishi Manula ameshindwa kuendelea na safari baada ya kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Algeria tukiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam,” imesema taarifa ya Simba kwenye mtandao wa klabu hiyo.

Simba ikiwa na wachezaji 22 imeondoka alfajiri ya Desemba 4,2024 kuelekea Algiers, Algeria, ambako watashuka dimbani Jumapili Desemba 8 kuwavaa CS Constantine katika mechi ya pili ya Kundi A la Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CL 2024/25).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news