Ajali yaua 14 na kujeruhi Mikese mkoani Morogoro

MOROGORO-Watu 14 wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya gari kubwa la mizigo kugongana uso kwa uso na gari dogo la abiria majira ya saa 2 usiku eneo la Mikese Mkoani Morogoro.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dkt. Daniel Nkungu wakati akiongea na waandishi wa habari Disemba 17, 2024 hospitalini hapo amesema, hospitali hiyo imepokea majeruhi saba.

Sambamba na miili ya watu 14 waliofariki katika ajali hiyo ambapo nane kati yao ni wanaume na sita ni wanawake hiyo ikiwa ni taarifa ya awali.

Dkt.Nkungu amesema, kati ya majeruhi saba wanaume ni wanne na watatu ni wanawake na kwa upande wa waliofariki Nane ni wanaume na sita ni wanawake kati yao mwili mmoja ni wa mtoto.

“Hapa hospitalini tumepokea majeruhi saba na miili ya watu 14 waliofariki,kati yao miili nane ya wanaume na miili sita ya wanawake,"amesema Dkt.Nkungu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news