RUVUMA- Walimu wanne wakiwemo Boniface Bosco Mapunda pamoja na dereva wa gari Vincent Alel Milinga wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Walimu hao ni Damas Damasi Nambombe, Domenica Abeat Ndau, Judith Joseph Nyoni na John Silvester Mtuhi wa Shule ya Msingi Lumalu.
Ajali hiyo ambayo imehusisha gari aina ya Prado T 647 CVR mali ya Vincent Alel Milinga kutoka kijiji cha Lumalu, Kata ya Upolo Wilaya ya Nyasa imetokea leo Desemba 28,2024 wakati wa safari kutoka Kijiji cha Lumalu kilichopo katika Kata ya Upolo kuelekea makao makuu ya Wilaya ya Nyasa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mheshimiwa Peres Magiri amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.