Akiba Commercial Bank PLC yazindua Kampeni ya Twende Kidijitali

DAR-Akiba Commercial Bank PLC imezindua Kampeni ya Twende Kidijitali ili kutoa suluhisho la kifedha kwa wateja wake kwa haraka popote walipo nchini.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 18,2024 na Kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha benki hiyo.

Kampeni hiyo imezinduliwa Desemba 12, 2024 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuboresha uzoefu wa wateja kupitia suluhisho la huduma za kifedha za kisasa, za haraka na za kuaminika

Pia,kampeni hiyo inahamasisha matumizi ya huduma za kidijitali kama vile ACB Mobile, Internet Banking, VISA na Akiba Wakala.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ACB Plc,Dkt Danford Muyango wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo amebainisha kuwa, wamejidhatiti kuboresha uzoefu wa wateja wao kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Dkt. Danford Muyango katika uzinduzi wa kampeni ya Twende Kidijitali.

Aidha,kwa mujibu wa Dkt.Muyango kampeni ya Twende Kidijitali pia imeungwa mkono na kampeni ya msimu wa sikukuu, "Twende Kidijitali, Tukuvushe January."

Amesema,lengo la kampeni hii ni mwendelezo wa azma ya Akiba Commercial Bank Plc ya kuongeza matumizi ya mifumo ya kidijitali ya benki na kuhamasisha wateja kufurahia manufaa ya kutumia teknolojia katika kutatua mahitaji yao ya kifedha.

"Kampeni pia inalenga kusaidia wateja kupitia kipindi cha Januari, ambacho mara nyingi kinakuwa kigumu kifedha,"amesema Dkt. Muyango, huku akisisitiza vigezo na masharti ya kampeni hiyo.

Aidha, ametaja masharti hayo kuwa ni pamoja na Idadi na Thamani ya Miamala ya Kidijitali ambapo Wateja watapimwa kulingana na idadi na thamani ya miamala yao kupitia huduma za kidijitali.

Pia, wateja walio na ushiriki mkubwa watakuwa na nafasi ya kushinda zawadi kuu za fedha taslimu.

Sharti jingine ni Uzoefu wa Kidijitali na Maoni ya Wateja ambapo Wateja watakaoshiriki kwa kutoa maoni ya thamani kuhusu huduma za kidijitali watapata nafasi ya kushinda katika droo ndogo.
Aidha, Wateja watakaowaalika wateja wengine kufanya miamala kwa njia ya ATM, POS, Wakala, Mobile Banking, au Internet Banking, wataweza kushinda zawadi

"Benki ya Akiba inawakaribisha wateja wote kushiriki nasi katika safari hii ya kidijitali. Kwa maelezo zaidi, tembelea matawi yetu au angalia majukwaa yetu ya kidijitali.Twendeni Kidijitali na Benki ya Akiba."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news