Arusha wamshukuru Rais Dkt.Samia, majiko ya Gesi ya Ruzuku yawafikia

ARUSHA-Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wamemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi wa kusambaza majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku ya 50% katika halmashauri hiyo.
Wametoa pongezi hizo Desemba 10, 2024 wakati wa utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko ya gesi yanayotolewa kwa bei ya ruzuku ya 50% na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano na Kampuni ya Lake Gas wilayani humo.
Walisema mradi umefika wakati mzuri kwani kwa sasa upatikanaji wa mkaa ni mgumu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kwamba inasababisha kupanda kwa gharama za maisha.

"Tumefurahi kufikiwa na mradi, suala la kuni na mkaa hapa kwa sasa ni shida; tunatumia muda mrefu kuwasha moto maana kuni ni mbichi," alisema Neema Rumas mkazi wa kijiji cha Siwandeti.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Siwandeti, Daniel Mitiweki amesema ujio wa mradi huo ni mkombozi wa mazingira kwani suala la ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa lilikithiri katika kijiji hicho lakini kufuatia mradi huo miti inakwenda kusalimika.

Akizungumza wakati wa zoezi la usambazaji na uuzwaji wa majiko hayo ya ruzuku wilayani humo, Msimamizi wa Mradi wa REA Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro na Arusha), Mhandisi Gift Kombe aliwasisitiza wananchi kuzingatia elimu inayotolewa ya matumizi sahihi ya majiko hayo ili yaweze kuleta tija inayokusudiwa ikiwa na kuendelea kujaza mitungi hiyo pindi inapoisha.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news