Askari mbaroni kwa kusababisha kifo cha mtoto Tabora

TABORA-Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu saba wakiwemo askari watatu wa Hifadhi za Misitu (TFS) na mgambo wanne baada ya kusababisha kifo cha mtoto mwenye umri wa miaka minne na kujeruhi mtu mmoja kwa risasi.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea tukio hilo mbele ya waandishi wa habari.

Amesema kuwa, tukio hilo limetokea Desemba 2 mwaka huu katika Kijiji Cha Igwisi Tarafa ya Kazaroho Wilaya ya Kaliua.

Pia,amesema kuwa siku hiyo majira ya saa 8 mchana Askari wa TFS wakiwa Doria katika Hifadhi ya Msitu wa Taifa Kigosi Moyowosi walikamata trekta lenye namba za usajili T 689 DCA Mali ya Sandu Kate lililokuwa linalima ndani ya hifadhi hiyo.

Amefafanua kuwa, wakiwa njiani kurudi kambini maeneo ya Igombambili kitongoji Cha Mpanda Mlowoka wananchi walijikusanya na kuzuia sskari hao wasipeleka trekta hilo kambini.

Askari hao wakiwa na silaha mbili aina ya AK 47 walifyatua risasi na kusababisha kifo cha mtoto huyo Grace Mussa (4) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya awali katika shule ya msingi Kalemela na kumjeruhi Zengo Sandu (47) ambapo risasi ilipenya chini ya kitovu na mkono wake wa kushoto.

Kamanda huyo amebainisha kuwa, uchunguzi wa daktari unaeleza kuwa chanzo cha kifo hicho ni kuvuja damu nyingi mtoto huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news