Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaja na mfumo wa malalamiko wa kidigitali

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuzindua mfumo wa kidigitali utakaomuwezesha mtumiaji wa huduma za kifedha kuwasilisha malalamiko, kuanzia Januari mwaka 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Ustawi wa Huduma Jumuishi za Kifedha wa BoT, Bi. Nangi Massawe amesema.
Ameyasema hayo leo Desemba 10,2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya siku mbili kuhusu mfumo wa malalamiko kwa wawakilishi wa taasisi za fedha jijini Dar es Salaam.

“Mfumo umetengenezwa na kukamilika tunaamini ifikapo Januari katikati, tutauzindua rasmi ili wananchi waweze kutuma malalamiko yao, ni muhimu sana kwa kupitia warsha hii tuhakikishe wote tumeuelewa vizuri na kuanza kuutumia kabla ya kuuzindua.”
Naye Kaimu Meneja Idara ya Ulinzi wa Watumiaji wa Fedha, (Financial Consumer Protection), Dkt.Hadija Kishimba amesema,BoT imeandaa warsha hiyo kwa taasisi za fedha ili kuuelewa mfumo kwani wao ndio wanaokutana na (walaji) wateja.

“Tubebe huu mfumo kwa sababu tunakwenda kusogeza huduma kwa wnanachi, tunataka mwananchi alalamike kupitia kiganja chake, alalamike kupitia computer yake.”
“Ninyi ndio wenye mfumo, nasema hivyo kwasababu ninyi ndio mnaokutana na wananchi, BoT imeandaa mfumo na tunapopeleka automation kwenye taasisi za fedha sio lengo la BoT kubaki na mfumo huo, lengo letu wananchi watumie ili na sisi tupate mrejesho.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news