Bilionea David Mulokozi anunua Helikopta binafsi

MANYARA-Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited,David Mulokozi amenunua ndege binafsi aina ya Helikopta ambapo ametua kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Stadium akiwa ameambatana na familia yake.
Mulokozi anaingia miongoni mwa Watanzania wachache wanaomiliki ndege binafsi ambapo amesema kuwa,kampuni yake imekua ikikua siku hadi siku na kuonesha vitu vya tofauti.

“Hakuna mtu alitegemea kuwa Manyara kunaweza kuwa na helikopta ni mambo mengi yanaanza ,Wafanyabiashara wengi wanajifunza, kila mtu anaruhusiwa kumiliki chombo hichi inawezekana."

Amesema kuwa, ndege hiyo itasaidia katika utoaji wa huduma katika kampuni yake inayojihusisha na uzalishaji wa vinywaji changamshi.

Mulokozi ameiomba Serikali ijenge uwanja wa ndege ili ndege nyingi zaidi ziweze kutua mkoani Manyara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news