WASHINGTON-Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton amelazwa hospitalini baada ya kupata homa.
Rais mstaafu wa Marekani, Bill Clinton.(Picha na Getty Images).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Chama cha Democrat,Angel Ureña kupitia mtandao wa X (Twitter).
Ureña amebainisha kuwa, Rais huyo wa 42 wa Marekani anaendelea kupokea matibabu huku hali yake ikionekana kuimarika.
Msemaji huyo amesema,Clinton alilazwa katika Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Georgetown huko Washington, DC siku ya Jumatatu jioni kwa ajili ya vipimo na uchunguzi baada ya kupata homa hiyo.