BoT yawapa mafunzo Kanda ya Ziwa kuhusu Mfumo wa Utatuzi wa Malalamiko

MWANZA-Benki na taasisi za fedha katika Kanda ya Ziwa zimepatiwa mafunzo kuhusu mfumo wa utatuzi wa malalamiko unaotarajiwa kuanzishwa rasmi na Benki Kuu ya Tanzania mapema mwakani.
Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 18 Desemba 2024 jijini Mwanza na kufunguliwa na Mkurugenzi wa Tawi la Benki Kuu ya Tanzania Mwanza, Bi. Gloria Mwaikambo.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Bi. Mwaikambo amesema: “Mfumo huu utarahisisha na kutatua changamoto za wateja wa huduma za kifedha kwa haraka na kwa uwazi kwa kuwa mteja atakuwa anaona malalamiko yake yalipofikia.”
Ofisa kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kisheria Benki Kuu, Bw. Kiwaligo Mtono, alitoa mada kuhusu mchakato wa uwasilishaji malalamiko akiwakumbusha washiriki kwamba, “malalamiko yoyote ambayo yameshafikishwa mahakamani, hayawezi kushughulikiwa na Benki Kuu.“

Aidha, Ofisa kutoka Kurugenzi ya Huduma Jumuishi za Fedha, Bw. Bondo Kafuku, alitoa mada kuhusu jinsi mfumo wa malalamiko unavyofanya kazi. Alieleza kuwa mfumo huo wa kidigitali, unaolenga kurahisisha mchakato wa kuwasilisha malalamiko kwa watumiaji wa huduma za kifedha, unatarajiwa kuanza kutumika rasmi kuanzia Januari mwaka 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news