KWA niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benki Kuu ya Tanzania itaendesha minada ya Dhamana za Serikali za MudabMfupi kwa siku 35, siku 91, siku 182,siku 364, na za muda mrefu (Hatifungani) za miaka 2, miaka 5, miaka 10, miaka 15, miaka 20 na miaka25 ambapo Hatifungani mpya zitatolewa na kufunguliwa tena kama ilivyoainishwa kwenye kalenda hii.
Kiwango cha riba pamoja na taarifanyingine za Hatifungani husika zitatangazwa kwenye tangazo la zabuni (Call for tender).
Minada ya Dhamana za Serikali itatolewa kwa utaratibu ufuatao, isipokuwa ikielezwa vinginevyo.