DAR-Uongozi wa Azam FC tarehe 10 Desemba,2024 umepokea ugeni mkubwa wa maofisa wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambao walifika kukagua miundombinu ya Uwanja wa Azam Complex, kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya CAF ya Wasichana chini ya umri wa miaka 17 Kanda ya CECAFA (GIFT).
Michuano hiyo inatarajia kufanyika hapa nchini kuanzia Januari 5 hadi 18, 2025, ambapo ukaguzi huo wa uwanja na miundombinu mingine ni sehemu ya maandalizi kwa waandaji kabla ya kuanza kutimua vumbi.