Chemba ya Wafanyabiasha Saudi Arabia yatambua mchango wa Dkt.Nchemba katika kukuza uwekezaji


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Riyadh, nchini Saudi Arabia, Bw. Ajian Saad Al-jlan, kwa kutambua mchango wake katika kukuza biashara na masuala ya uwekezaji nchini Tanzania, kupitia wadhifa wake wa Waziri wa Fedha. Tukio hilo limefanyika wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Jukwaa lililoandaliwa na Serikali kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini humo, likiwa na lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa Saudi Arabia ili kuvutia mitaji na teknolojia vitakavyochochea ukuaji wa uchumi na kukuza kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Mawaziri wengine waliotunukiwa zawadi hizo ni Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Suleiman Jafo, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, Waziri wa Nchi Ofisi ya rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji-Zanzibar, Mhe. Shariff Ali Shariff na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news