Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) chazindua Kamati ya Maadili ya Tafiti (ISWREC)

DAR-Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) kimezindua Kamati ya Maadili ya Tafiti (Institute of Social Work Research Ethics Committee-ISWREC) katika hafla maalum iliyofanyika Chuo cha Ustawi wa Jamii – Kampasi ya Kijitonyama, Dar es Salaam tarehe 12 Desemba, 2024.
Katika hafla hiyo, Bi Joyce Ikingura alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa ISWREC kupitia mchakato wa uchaguzi kwa uwazi.
Baada ya uchaguzi huo, Mkuu wa Chuo, Dkt. Joyce Nyoni, kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa ISWREC Bi Joyce Ikingura walizindua rasmi kamati hiyo na Muongozo wa Ufanyaji wa Tafiti, ambao utatumika kama mwongozo wa kuhakikisha tafiti zote zinazofanyika Chuo cha Ustawi wa Jamii zinazingatia maadili ya kitafiti.
Uzinduzi wa ISWREC unadhihirisha dhamira ya Chuo cha Ustawi wa Jamii katika kuhakikisha tafiti za kitaaluma zinafanyika kwa njia inayoheshimu maadili ya kitafiti na haki za washiriki katika kuchangia maendeleo ya kijamii na kitaaluma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news