DCEA yatoa elimu kwa mamia ya wanafunzi Arusha

ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 29-30 Novemba 2024 imeadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani kwa kutoa elimu kinga kuhusu madhara ya dawa za kulevya kwa zaidi ya wanafunzi 1,050 wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Shule ya Sekondari Losinoni wilayani Arumeru.
Wanafunzi walihamasishwa kuhusu uhusiano wa matumizi ya dawa za kulevya na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Homa ya Ini B na C, pamoja na kutokuwanyanyapaa waraibu wa dawa za kulevya.
Katika Shule ya Losinoni, elimu hiyo ilihitimishwa na kukabidhiwa mipira miwili kwa shule hiyo ili kuhamasisha vijana kushiriki michezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news