DAR-Saa chache baada ya kuibuka malumbano mitandaoni kuwa, Diamond Platnumz hakutumbuiza katika Tamasha la Furaha City huko Nairobi nchini Kenya kutokana na sababu wanazozifahamu wenyewe.
Huku wasanii wa Kenya wakidai, wasanii wa Tanzania wanapendelewa zaidi, Diamond Platnumz ameibuka na kujibu hoja ya mchekeshaji wa Kenya,Eric Omondi ambaye amedai kuwa, wasanii wa Kenya kila siku wamekuwa hawapewi thamani kwenye shows zao.
"My Brother Eric, mafanikio hayaji kwa kuwawekea chuki wengine, bali yanakuja kwa kuongeza juhudi kisha Mungu nae atakubariki...
"Wewe ni mmoja ya mfano mzuri kwenye hili, ulishakuja zaidi ya mara 10 Tanzania kufanya shows as the headliner na sikuzote ulipokewa kwa upendo, hukuwahi kusikia Standup Comedians wakikuletea chuki ama kuskia wakisema wanaonewa wala campaign za “We want 75% Tanzanian Comedians.
"Walijiassess wakaona nini wafanye ili nao kufanikiwa, wakaweka bidii, zikaanzishwa ChekaTu, Watu Baki na Platforms mbalimbali za Standup Comedy ambazo zikazalisha Standup Comedians wengi, na leo hii nao wananufaika na kazi zao.
Juzi tu,alikuja Bien Tanzania na watu wamempokea kwa upendo na kufanya kazi na wasanii .balimbali...
"Afrika Mashariki ni nchi zinazoishi kwa upendo na ushirikiano, jitahidi kuhamasisha upendo na ushirikiano na kuweka bidii, instead ya kuwafunza wasanii watuwekee chuki maana sio solution ya kufanikiwa,” amebainisha Diamond Platnumz.