ADDIS ABABA-Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshiriki kikao cha Mawaziri cha kujadili masuala ya Maendeleo ya Uchumi, Biashara, Utalii, Viwanda na Madini kwenye Umoja wa Afrika (AU) tarehe 13 Desemba, 2024 jijini Addis Ababa, nchini Ethiopia.
Kikao hicho cha Mawaziri kilitanguliwa na kikao cha wataalam kilichofanyika tarehe 11 na 12 Desemba, 2024.
Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili Agenda mbalimbali ikiwemo Agenda:
i. Rasimu ya tathmini ya utayari kuelekea Umoja wa Forodha wa Afrika/Soko la Pamoja;
ii. Rasimu ya Mkakati wa kubadilisha na kukuza mauzo ya Nje ya Afrika; na
iii. Rasimu ya Mkakati wa Madini ya Muhimu Afrika.
Akizungumzia katika kikao hicho Dkt. Kiruswa alilisitiza kuwa kutokana na uhitaji wa Madini hayo muhimu duniani sambamba na ukuaji wa teknolojia ni vyema kuwepo na mkakati wa uvunaji wa madini hayo muhimu Barani Afrika ambapo mkakati huo utasadia kwa nchi wanachama wa Umoja wa nchi za Afrika kutengeneza mikakati yao inayoendana na mkakati mkubwa wa Afrika.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mhe. Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara na watalaamu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Picha na matukio mbalimbali wakati wa Kikao cha Waheshmiwa Mawaziri kutoka nchi zote za Bara la Afrika.