UONGOZI wa timu ya Fountain Gate Football Club umevunja benchi lote la ufundi lilokuwa likiongozwa na kocha mkuu Mohamed Muya.
Hatua hiyo imechukuliwa muda mfupi baada ya timu hiyo kupoteza kwa goli 5-0 katika Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam.
"Klabu inawashukuru kwa mchango wao ndani ya timu na kuwatakia kila la kheri," taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate imesema.