NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange amezitaka halmashauri zenye miradi yenye kujiendesha kama masoko na stendi kuhakikisha zinawahamasisha wananchi kuitumia miradi hiyo ili iwe na tija na manufaa kwa jamii na taifa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange akikata utepe kwenye mkataba wa ujenzi wa soko kuu la mazao ya nafaka ambalo litajengwa eneo la Kanondo kupitia fedha za mradi wa TACTIC, kabla ya kushuhudia mkataba huo ukisaniwa.
Dkt. Dugange ametoa malekezo hayo akiwa mjini Sumbawanga kwenye ukumbi wa Nazareti, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa soko kuu la mazao ya nafaka ambalo litajengwa eneo la Kanondo kupitia fedha za mradi wa TACTIC.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange akionesha mkataba wa ujenzi wa soko kuu la mazao ya nafaka ambalo litajengwa eneo la Kanondo kupitia fedha za mradi wa TACTIC, mara baada ya mkataba huo kusainiwa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange akionesha mkataba wa ujenzi wa soko kuu la mazao ya nafaka ambalo litajengwa eneo la Kanondo kupitia fedha za mradi wa TACTIC, mara baada ya mkataba huo kusainiwa.
Dkt. Dugange amesema wakulima wengi wamekuwa wakipata changamoto ya kutunza mazao yao katika maeneo ambayo yanaharibika hivyo ujenzi wa soko hilo na masoko mengine kupitia mradi wa TACTIC umekuja wakati muafaka.
“Soko hili likikamilika muwe na mpango wa kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi na wakulima ili waweze kulitumia soko hili kufanya biashara na kujipatia faida itakayowawezesha kujijenga kiuchumi na kuchangia pato la taifa,” Dkt. Dugange amesisitiza.
Aidha, Dkt. Dugange amewaasa wakurugenzi wanaotekeleza miradi ya TACTIC kuhakikisha mikataba ya utekelezaji inasainiwa kwa wakati na kusimamia kikamilifu utekelezaji wake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Nazareti Manispaa ya sumbawanga, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa soko kuu la mazao ya nafaka ambalo litajengwa eneo la Kanondo kupitia fedha za mradi wa TACTIC.
Baadhi ya wananchi wa Sumbawanga wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange (hayupo pichani) wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa soko kuu la mazao ya nafaka ambalo litajengwa eneo la Kanondo kupitia fedha za mradi wa TACTIC.
Dkt. Dugange ameongeza kuwa, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kipaumbele kwa wakandarasi wazawa kupatiwa miradi ya TACTIC, hivyo wakandarasi wazawa wanapaswa kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi na uzalendo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono uamuzi wa Mhe. Rais kuwapatia kandarasi.
Jumla ya shilingi bilioni 7.4 zitakumika katika ujenzi wa soko kuu la mazao ya nafaka ambalo litajengwa eneo la Kanondo katika Manispaa ya Sumbawanga, ambapo kwa mujibu wa mkataba uliosaniwa soko hilo litakamilika Disemba 2025.