NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali itajenga shule, zahanati, sekondari na kituo cha afya ili kusogeza huduma za kijamii kwenye makazi mapya ya waathirika wa maporomoko ya tope Hanang mkoani Manyara.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi hati na funguo ya nyumba mmoja wa waathirika wa maporomoko ya tope. Mhe. Majaliwa amekabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope wilayani humo.
Mhe. Kassim Majaliwa amesema hayo akiwa Wilayani Hanang, wakati akikabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope wilayani humo, ambazo zimejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu kwenye Kitogoji cha Waret kijiji cha Gidagamowd.
“Tunataka wananchi hawa wawe na mwingiliano na wengine,waendelee kuishi hapa na wapate huduma muhimu za kijamii na ndio maana tutajenga shule, zahanati, sekondari na kituo cha afya,” Mhe. Majaliwa amesisitiza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi katika Kitogoji cha Waret kijiji cha Gidagamowd Wilayani Hanang (hawapo pichani), kabla ya kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope wilayani humo.
Mmoja wa waathirika wa maporomoko ya tope wilayani Hanang akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya Mhe. Waziri Mkuu kumkabidhi nyumba ya kuishi mwananchi huyo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahi na wananchi waliojitokeza katika Kitogoji cha Waret kijiji cha Gidagamowd Wilayani Hanang (hawapo pichani), mara baada ya kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope wilayani humo.
Muonekano wa baadhi ya nyumba zilizokabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa waathirika wa maporomoko ya tope Hanang, nyumba hizo 109 zimejengwa katika Kitogoji cha Waret kijiji cha Gidagamowd Wilayani Hanang.
Wananchi wa Hanang wakisikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika Kitogoji cha Waret kijiji cha Gidagamowd, kabla ya Mhe. Waziri Mkuu kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope wilayani humo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akishuhudia kikundi cha burudani kikitumbuiza (hakipo pichani) alipowasili katika Kitogoji cha Waret kijiji cha Gidagamowd Wilayani Hanang kwa ajili ya kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope wilayani humo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI alipowasili katika Kitogoji cha Waret kijiji cha Gidagamowd Wilayani Hanang ili kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope wilayani humo.
Aidha, Mhe. Majaliwa amefafanua kuwa, kati ya nyumba hizo 109 alizozikabidhi kwa waathirika wa maporomoko ya tope, nyumba 73 zimegharamiwa na Serikali, nyumba 35 zimegharamiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania na nyumba moja imegharamiwa na Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT).
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa, nyumba zote hizo zimejengwa kwa uratibu mzuri wa timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Hanang pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.
Sanjari na hilo, Mhe. Majaliwa ameipongeza na kuishukuru TARURA kwa ujenzi mzuri wa barabara kwenye eneo hilo ambalo zimejengwa nyumba 109 za waathirika wa maporomoko ya tope na kuongeza kuwa toka amefika na kuanza ukaguzi wa nyumba hajaona barabara iliyoteleza licha uwepo wa mvua iliyokuwa ikinyesha.
“Mhe. Waziri wa TAMISEMI na TARURA yako mmefanya kazi nzuri sana ya ujenzi wa barabara kwenye nyumba hizi 109, hivyo jukumu mlilobakia nalo ni kutuwekea lami hivyo jaribu kuangalia kwenye vifungu vyako vya bajeti ili barabara ziwekwe lami,” Mhe. Majaliwa ameeleza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa waathirika wa maporomoko ya tope wilayani Hanang ambao amewakabidhi hati na funguo za nyumba 109 zilizongenjwa kwa ajili yao.
Baadhi ya waathirika wa maporomoko ya tope wilayani Hanang wakisikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika Kitogoji cha Waret kijiji cha Gidagamowd, kabla ya Mhe. Waziri Mkuu kuwakabidhi nyumba 109 za kuishi.
Maporomoko ya tope wilayani Hanang yaliyotokea Desemba 7, 2023 katika mji mdogo wa Katesh pamoja na vijiji jirani yalipelekea baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kupoteza nyumba za kuishi, hivyo Serikali ilichukua hatua ya kukabiliana na changamoto hiyo na hatimaye Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amekabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko hayo.