IJP Wambura afanya mabadiliko

DODOMA-Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IJP), Camillus M. Wambura amefanya mabadiliko madogo kwa Wakuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambapo amemhamisha Naibu Kamishna wa Polisi,DCP Ramadhani Ng’anzi kutoka Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania kwenda Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma.

Ng’anzi atakuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Maadili ya Jamii na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP William Mkonda ambaye alikuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam.
IJP Wambura amemhamisha pia aliyekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Boniphace Mbao kutoka Dodoma kuja kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam na aliyekuwa Mkuu wa Elimu kwa Umma Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Michael Deleli amemhamishia Makao Makuu ya Polisi Dodoma kuwa Kaimu Mkuu wa Maadhimisho ya Kitaifa.

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nassoro Sisiwaya aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania amemhamishia Mkoa wa Kilimanjaro kwenda kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news