ARUSHA-Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali majenerali, naafisa na askari wa JWTZ.
Hafla hiyo imefanyika Desemba 2,2024 jijini Arusha ambapo nishani hizo ni pamoja na Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne.
Pia, Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.
Jenerali Mkunda amewavisha nishani ya Jumuiya ya SADC Maafisa na Askari walioshiriki Ulinzi wa Amani Nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa Jumuiya hiyo ambapo akiongea na Wanajeshi Kanda ya Arusha, Jenerali Mkunda amemshukuru Rais kwa kuwatunuku Nishani hizo.
Hata hivyo,amewataka wanajeshi kote nchini kuviishi viapo vyao walivyoapa, kufanya kazi kwa ngugu zote kwa uhodari, uaminifu, utalii na nidhamu ili kuweza kuilinda Nchi, kulinda Katiba na kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.