Job opportunity from Mbinga Farmers Cooperative Union (MBIFACU) Limited

MBIFACU LTD ni chama kikuu cha Ushirika wa Mazao Mkoa wa Ruvuma kilichoanzishwa na vyama vya Msingi vilivyo sajiliwa kwa lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za vyama vya Msingi vilivyopo ndani ya Mkoa wa Ruvuma vinavyojishughulisha na mazao mchanganyiko zao kuu ikiwa ni kahawa.

Madhumuni ya kuanzishwa kwa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima Mbinga ni kuinua, kuimarisha na kuendeleza hali ya kiuchumi na kijamii kwa kufanya mipango ya kuendeleza shughuli za kilimo na masoko zinazoendeshwa na vyama wanachama kwa kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika. Ili kufanikisha madhumuni haya, Chama Kikuu kitafanya yafuatayo:-

  • Kuhamasisha na kuendeleza shughuli za Ushirika kwa wanachama wake, kuhamasisha vyama vya msingi vya mazao ya kilimo cha Kahawa, Korosho, mazao mchanganyiko na mazao ya chakula vilivyopo katika eneo lake kujiunga na Chama Kikuu na kusaidia Vyama wanachama katika kujiendeleza ili kuwa vyama vyenye misingi imara ya kiuchumi na vinavyoweza kujitegemea.
  • Kutoa elimu ya kilimo cha kibisahara chenye kufuata kanuni bora za kilimo pamoja na misingi imara.
  • Kusaidia vyama wanachama katika kuongeza uzalishaji wa mazao yote.
  • Kuwezesha ukusanyaji na uuzaji wa mazao ya wanachama kwa mfumo wa stakabadhi  ya ghalani pamoja na utafutaji wa masoko ya uhakika na yenye tija kwa mazao ya wanachama.
  • Kununua, kukodi na kustawisha ardhi, majengo na vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi yake pamoja na wanachama
  • Kukodi, kununua na kuendesha mitambo, maghala, maofisi na magari ili kuweza kutoa huduma inayohitajika kwa wanachama wake katika shughuli za kilimo..
  • Kuviwakilisha vyamavya msingi kukusanya na kuuza mazao ya wanachama wake, pia kusambaza  pembejeo pamoja na bidhaa nyingine ambazo ni muhimu kwa kilimo kwa lengo la kutoa huduma nzuri na bora kwa wanachama wake.
  • Kununua Hisa katika vyama vingine vya Ushirika vyenye dhima ya kikomo, au katika mashirika ya biashara na vyombo vingine vya umma baada ya kupata kibali cha Mrajis wa Vyama vya Ushirika kwa maandishi.
  • Kusimamia kikamilifu fedha zote za mazao zinazotolewa na Chama Kikuu kwa ajili ya ununuzi mazao.
  • Kutoa ushauri, kuelekeza na kusimamia, endapo ni lazima, vyama wanachama wakati wa kutayarisha makisio ya mapato na matumizi ili yawasilishwe kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika kwa kupata kibali chake.
  • Kuanzisha na kuendeleza mafunzo kwa wanachama na watendaji wa Chama Kikuu kuhusu shughuli zao katika Chama.
  • Kuwa kitovu cha uratibu na utafutaji wa masoko ya mazao ya wanachama pamoja na upatikanaji wa taaluma ya masoko kwa wanachama.
  • Kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo, zana bora za kilimo na mahitaji mengine kwa ajili ya kusambaza na kuwauzia vyama wanachama kwa bei nafuu kwa manufaa ya wanachama wao.
  • Chama kinaweza kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi iwapo ni lazima baada ya kufanya upembuzi yakinifu kwa manufaa ya Chama Kikuu na wanachama.
  • Kuanzisha mradi wa usindikaji wa mazao ya vyama wanachama au kusaidia vyama wanachama kuanzisha miradi ya namna hii.
  • Kutoa elimu ya Ushirika kwa wanachama, wajumbe wa Bodi na watendaji kuhusu dhana ya ushirika na manufaa yake, ujasiriamali na tasnia nyingine zinazohusiana na miradi inayoendeshwa na kutekelezwa na wanachama wake.
  • Kwa ujumla kufanya mambo yote yaliyo halali na ambayo ni lazima au muhimu katika kuendeleza madhumuni yaliyotajwa hapo juu pamoja na mengine kama ilivyo chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Namba 6 ya mwaka 2013 na kanuni zake.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news