Katazo la kutoa mikopo bila kuwa na leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

BENKI Kuu ya Tanzania inapenda kuukumbusha umma kuwa, kwa mujibu wa Kifungu cha16 (1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, ni kosa kwa taasisi, kampuni na watu binafsi kujihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila kuwa na leseni kutoka BenkiKuu ya Tanzania. 

Aidha, Kifungu cha 16(2) (a) cha Sheria hiyo kimeainisha adhabu inayopaswa kutolewa kwa kuendesha biashara ya kukopesha bila kuwa na leseni ikiwa ni pamoja na kutozwa faini isiyopungua Shilingi milioni 20 au kifungo cha muda usiopungua miaka miwili au vyote viwili kwa pamoja.

Hivyo basi, Benki Kuu inapenda kuusisitiza Umma kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au mtu binafsi ambaye hana leseni. 

Endapo taasisi au mtu binafsi anataka kufanya biashara ya ukopeshaji anatakiwa kufuata taratibu husika za kuomba leseni kutoka Benki Kuu ili apewe kwa mujibu wa Sheria. 

Ni muhimu mtu anapotaka kukopa, atumie taasisi zenye leseni ya Benki Kuu ili kuhakikisha kuwa huduma anayopata ni salama na inayozingatia Sheria za nchi.

Aidha, kuna baadhi ya taarifa katika mitandao ya kijamii zinazohusisha alama za wanyama kama vile Kobe na Nyoka katika utoaji wa mikopo, jambo hilo ni kinyume cha Sheria na maadili ya utoaji wa huduma za kifedha. 

Hivyo, wananchi wanashauriwa kupuuza taarifa hizo na kutokujihusisha nazo kwa kuwa hazijapewa leseni hapa nchini.

Orodha ya taasisi zenye leseni za kukopesha zilizotolewa na Benki Kuu pamoja na leseni za mikopo ya kidijiitali zipo kwenye tovuti ya Benki Kuu, kupitia ukurasa wa:


Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na: Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania, 2 Mtaa wa Mirambo, S.L.P 2939, 11884 Dar es Salaam, Simu Na. +25522 223 5586; Barua Pepe: info@bot.go.tz au botcommunications@bot.go.tz

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news