ZANZIBAR-Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale,Dkt. Aboud Suleiman Jumbe ameongoza kikao na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo vya Wizara na Wadau mbalimbali wa Sekta za Umma na Sekta Binafsi.
Ni kwa ajili ya kutoa maoni juu ya Kutathmini Utekelezaji wa Mkataba wa Utoaji Huduma wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale (Client Service Charter).
Pia,lengo kuu ni kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa Wananchi zinakidhi viwango vilivyowekwa.
Kikao hicho kimefanyika Disemba 2,2024 katika Ofisi za Wizara iliyopo Kikwajuni - Zanzibar.
Mkataba huu ni msingi wa uwajibikaji kwa umma na wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii katika Utoaji wa Huduma,Uwepo wa Uwazi, Uwajibikaji wa huduma yenyewe, Uadilifu, Mapambano dhidi ya Rushwa.
Pia,Jinsi ya kushughulikia Malalamiko ya Wananchi na Mapokezi yenyewe kwa Wananchi na Wadau wote wa Sekta ya Utalii.